UGONJWA WA KISUKARI,CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE,ATHARI NA MATIBABU YAKE ASILI

Ugonjwa wa Kisukari ni hali ya Kiwango cha Sukari kuzidi kwenye damu kutokana na tezi za kongosho kushindwa kuzalisha vichocheo vya kutosha vya insulin, au mwili kupoteza sifa na uwezo wa kuvitumia vichocheo vya insulin vyenye kazi ya kudhibiti kiwango cha Sukari mwilini.






=====

Kisukari ni ugonjwa unaoambatana na hali ya uwepo wa sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu.

Hutokea baada ya tezi za kongosho kushindwa kuzalisha vichocheo vya kutosha vya insulin, au mwili ukipoteza sifa na uwezo wa kuvitumia vichocheo vya insulin vinavyo zalishwa hivyo kufanya ongezeko kubwa la sukari litokee kuliko kiwango cha kawaida kinachotakiwa.




Insulin ndiyo vichocheo vinavyotumiwa na mwili katika kudhibiti ongezeko la sukari.

AINA ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kuna aina nyingi za kisukari, lakini wataalam hupenda kuugawa ugonjwa huu kwenye aina kuu tatu ambazo ni kisukari aina ya kwanza, kisukari aina ya pili pamoja na kisukari cha ujauzito.

Aina ya kwanza ya kisukari: hutokea baada ya mwili kukosa sifa na uwezo wa kuzalisha vichocheo vya insulin. Mara nyingi husababishwa na mwili wenyewe kuzishambulia seli zinazozalisha vichocheo hivi. Walau asilimia 10 ya wagonjwa wote wa kisukari huwa wapo kwenye kundi hili. Hufahamika pia kama kisukari kinachotegemea insulin


Aina ya pili ya kisukari: hutokea kwa watu ambao miili yao huzalisha vichocheo vya insulin, lakini huwa sugu kiasi cha kushindwa kuvitumia kikamilifu katika kudhibiti sukari. Walau asilimia 90 ya wagonjwa wote wa kisukari huwa wapo kwenye kundi hili. Hufahamika pia kama Kisukari kisichotegemea insulini.


Kisukari cha ujauzito hutokea wakati wa ujauzito pekee. Husababishwa na baadhi ya vichocheo ambavyo mwili wa mwanamke huvitengeneza ili kumlinda mtoto. Aina hii ya kisukari mara nyingi huisha baada ya kujifungua

VITU HATARUSHI KWA MGONJWA WA KISUKARI

Baadhi ya mambo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari. Miongoni mwake ni-
Kutoka kwenye familia yenye historia ya uwepo wa ugonjwa huu
Kuwa na uzito mkubwa
Umri wa zaidi ya miaka 45
Kutokufanya kazi yoyote au mazoezi yanayoongeza utimamu wa mwili
Kuwa na shinikizo kubwa la damu na mafuta mengi
Kuwa na ujauzito
Uwepo wa changamoto kwenye mfumo wa taarifa za mfumo wa kinga za mwili unaoweza kushambulia tezi za kongosho
Kuwa mvutaji wa sigara


DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Dalili za kisukari husababishwa na uwepo wa sukari nyingi mwilini ambazo huufanya mwili uanze kuonesha tabia hasi. Baadhi ya dalili hizo ni
Kuhisi njaa kila mara
Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara
Kuhisi kiu mara kwa mara
Kupungua uzito wa mwili na kukonda
Kupatwa na vidonda visivyo pona kirahisi
Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati
Kupungua kwa uwezo wa macho katika kuona
Kupungua kwa hamu na uwezo wa mwanamme kwenye kushiriki tendo la ndoa
Maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa mkojo, miwasho sehemu za siri na fangasi wa mara kwa mara

ATHARI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kisukari ni mojawapo ya magonjwa yanayo ongoza kwa kuua watu wengi duniani kila mwaka pamoja na kusababisha ulemavu na utegemezi wa kudumu.

Pia, huchangia kwa kiasi kikubwa upofu, magonjwa ya moyo, maambukizi makali mwilini yanayoweza kusababisha vidonda visivyopona, maumivu ya kudumu ya miguu, ugonjwa wa figo, kiharusi, kudumaa kwa afya ya uzazi kwa jinsia zote, kujifungua kabla ya wakati pamoja na kifafa cha ujauzito.

Kati ya mwaka 2000 – 2016, kulikuwa na ongezeko la asilimia 5 la vifo vya mapema duniani vilivyo sababishwa na kisukari.

Mwaka 2019, ugonjwa wa kisukari ulishika namba 9 duniani katika kusababisha vifo ambapo takriban watu 1.5 M walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu.

Matibabu na Ushauri
Matibabu ya kisukari huhusisha mazoezi, lishe, kudhibiti uzito pamoja na matumizi ya dawa.






Kutokana na aina husika ya kisukari, mhudumu wa afya atatoa dawa pamoja na ushauri wa namna bora ya kutumia dawa hizo. Mfano wa dawa hizo ni Metformin, glibenclamide, insulin n.k
Shiriki mazoezi, husaidia kuunguza nishati pamoja na kupunguza usugu wa mwili katika kutumia vichocheo vya insulin.
Lishe huchukua sehemu kubwa ya matibabu kwa kuwa karibia kila chakula hugeuzwa kuwa sukari mwilini. Uchaguzi wa vyakula vyenye kiasi kidogo cha mafuta na wanga, nafaka nzima, nyuzi lishe nyingi, matunda pamoja na mboga za majani hushauriwa.
Ni muhimu kudhibiti ongezeko la uzito wa mwili. Ukubwa wa athari za kisukari mara nyingi huenda sambamba na kiasi cha uzito alio nao mgonjwa.
Usivute sigara
Punguza matumizi ya pombe
Punguza matumizi ya chumvi hadi kijiko kimoja kwa siku

Kisukari ni ugonjwa wenye kutibika kwa dawa za asili hasa pale utakapobahatika kupata dawa ya uhakika katika kutibu kisukari mfano wa dawa za uhakika zenye kuondosha kabsa kisukari ni dawa ya asili iitwayo DM POWDER

Wasiliana na mimi kwa maelezo zaidi

0755162724
Dr Liwaya

Dar es salaam, Ilala 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.