TATIZO LA KUPATA CHOO KIGUMU NA SULUHISHO LAKE
Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.
Kufunga kwa choo au kupata choo kigumu ndiyo chanzo kikubwa cha ugonjwa wa bwasiri kwa Tanzania, na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku.
Zifuatazo ni dawa 10 mbadala zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:
1. Mafuta ya Zeituni
Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo. Yana ladha nzuri mdomoni na ni dawa pia.Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni, changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.
2. Juisi ya Limauo
Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo. Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.
3. Mazoezi ya kutembea
Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida, basi jitahidi uwe mtu wa kutembea tembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima.Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembea tembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
4. Vyakula vya nyuzi (fiber)
Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umuhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla.
Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni muhimu kula kila siku, kadhalika tumia unga au mbegu za maboga.
5. Aloe Vera
Ni muhimu utumie Aloe Vera fresh kwa kuchanganya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya Aloe Vera
6. Baking soda
Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo, na pia inasaidia kupunguza asidi mwilini.Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.
7. Mtindi
Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.
8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)
Fanya mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi muhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.
9. Matunda
Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo, pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.
10. Maji ya Kunywa
Maji ni uhai. Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji!.
Hakuna maoni