ZIJUE FAIDA,MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU



               
MAGONJWA YANAYOTIBIKA KUPITIA KITUNGUU SAUMU
  1. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
  2. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
  3. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
  4. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
  5. Huondoa Gesi tumboni
  6. Hutibu msokoto wa tumbo
  7. Hutibu Typhoid
  8. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
  9. Hutibu mafua na malaria
  10. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
  11. Hutibu kipindupindu
  12. Hutibu upele
  13. Huvunjavunja mawe katika figo
  14. Hutibu mba kichwani
  15. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
  16. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
  17. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
  18. Hutibu maumivu ya kichwa
  19. Hutibu kizunguzungu
  20. Hutibu shinikizo la juu la damu
  21. Huzuia saratani/kansa
  22. Hutibu maumivu ya jongo/gout
  23. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
  24. Huongeza hamu ya kula
  25. Huzuia damu kuganda
  26. Husaidia kutibu kisukari
  27. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
  28. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu

FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.








MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka:                                                                                                                                  
kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.


Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.