Hatua 4 za Kutibu Kiungulia

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaoteseka sana na kiungulia basi fahamu kwamba kupambana na tatizo hili inahitaji kujua chanzo chake na kisha uchukue hatua katika kuondoa visababishi vya tatizo. Baadhi ya sababu zinazokufanya uendelee kuwa muhanga wa kiungulia ni pamoja na lishe mbaya, kutofanya mazoezi, kuzeeka, unatumia vidonge kwa muda mrefu ambavyo vinabadili mazingira ya uchakataji wa chakula, ama una msongo wa mawazo uliokutafuna kwa muda mrefu.

Kiungulia ni Kitu Gani

Kiungulia kwa kitaalamu tunaita heartburn ni hali ya kukera inayosababisha maumivu makali kwenye kifua na upande wa juu wat umbo. Hali hii inaendana kwa ukaribu wa kupanda kwa tindikali(acid reflux). Kuantofauti kati ya acid reflux na heartburn, acid reflux ni kitendo cha kupanda kwa tindikali kutoka tumbo kurudi juu kwenye umio la chakula na kusababisha maumivu ya kifua ambayo sasa tunaita ni Heartburn. Kwahiyo acid reflux inaweza kusababisha heartburn. Kiungulia ni kitendo cha kawaiada kwa watu wengi na inatokea kwa kila mtu, lakini kama tu haiambatani na maumivu makali ya kifua, kama maumivu yakizidi kuwa makali na yanatokea mara kwa mara hapo ndipo tatizo huanza. Kama tatizo likiendelea zaidi basi hufikia hatua ya tatu na kuitwa gastroesophageal reflux disease kwa kifupi(GERD), kwa hiyo kadiri kiungulia kinachukua muda mrefu mapaka kuathiri tishu za umio tunaita GERD, GERD ni hatari zaidi kwa inaweza kusababisha saratani ya koo la chakula. Unapoona dalili hizi basi fahamu kwamba umeingia hatua ya ugonjwa kuitwa GERD. Dalili hizi ni kama kupata shida kwenye kumeza chakula na vinywaji, kupata kikohozi kikavu chenye maumivu makali wakati fulani, kupata shida ya kupumua wakati flani, . mara nyingi dalili hizi za GERD huwa zinakuja usiku, kila siku ama kila baada ya siku kadhaa kwa mwezi.

Dalili za Kiungulia (heartburn)

Dalili kuu za kuonesha kwamba tayari una kiungulia ni kama

  • Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea baada tu ya kula
  • Mdomo kuwa mchachu muda mwingi
  • Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu
  • Mdomo kukauka
  • Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
  • Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali
  • Tumbo kujaa na kujamba sana baada ya kula
  • Tumbo kuunguruma na
  • Kukosa hamu ya chakula na kichefuchefu.

Mazingira Hatarishi ya kupata Kiungulia Pamoja na Visababishi vyake

Kiungulia na kupanda kwa tindikali husababishwa na matatizo kwenye mfumo wa usagaji chakula kama tumboni, kwenye valve zinazozuia chakula kurudi kilikotoka na pengine shida kwenye umio la chakula. Japo kisababishi halisi cha kiungulia bado hakijajulikana, ila maumivu yanayotokea kwenye kifua ni kutokana na tindikali ya tumboni inapopanda na kuunguza tishu za umio. Kundi kubwa la watu wenye shida ya usagaji wa chakula ni kutokana a kwamba wana tindikali kidogo kwenye tumbo na pia wanakula vyakula vinavyoongeza utundikali, ili kupata suluhu ya tatizo hili unahitajika kuweka msawazo kati ya tindikali na alkali tumbo yaani pH. Wakati mwingine ni vigumu kujua kiungulia chako kinasababishwa na nini hivo inahitaji kujaribu na kuchunguza mwili wako kwa mwili, tazama ni vyakula gani ama kitu gani ukitumia vinaleta shida zaidi. Vifuatavyo ni vyakula na mazingira yanayokusababishia uwe na kiungulia

  • Lishe mbovu: wanaokula zaidi vyakula vilivyosindikwa, sukari, chocolate, cyakula vyenye caffeine kama kahawa wapo kweye hatari zaidi ya kupata kungulia.
  • Upungufu wa madini kama Mgnesium na Potassium
  • Ulaji wa mlo mkubwa badala ya kula kidogo kidogo kwa kuweka gape la muda hasa unapokarbia kulala
  • Kuwa na alegi au mzio kwa vyakula baadhi
  • Maisha ya kizembe, kwa kutumia muda mwingi ukiwa umekaa pasipo kushugulisha mwili wako
  • Uzito mkubwa na kitambi
  • Msongo wa mawazo kupita kiasi ni chanzo cha kiungulia
  • Matumizi ya vidonge kwa muda mrefu, hasa antibiotics, ibuprofen na asprini
  • Kufanya mazoezi kupita kiasi bila kupata muda wa kupumzika kitendo kinachoweka presha kubwa sana kwenye tumbo.
  • Wamama wajawazito wako kwenye hatari zaidi ya kupata kiungulia
  • Wazeee na wenye umri mkubwa
  • Wenye historia ya kuwa na ugonjwa wa hernia

Tiba ya Kisasa kwa Kiungulia

Unapofika hospitali madactari wengi hupendekeza upate dawa za antiacid ili kupunguza makali ya dalili, japo kadiri unavoendelea kutumia dawa hizi unaongeza magonjwa mengine ya mfumo wa chakula na kuharibu bacteria wazuri walioko tumboni, antiacid zinaweza kusababisha kukosa choo ama kupata choo kw shida, kuharisha, matatizo kwenye figo na kushuka kwa kinga ya mwili.

Hatua 4 za Kutibu Kiungulia na Dalili zake kwa Kutumia Lishe na Kubadili Mtindo wa maisha.

  1. Kula lishe nzuri ya uhakika na pia tupilia mbali vyakula vinavyoongeza tatizo
    tafiti mbalimbali zinashauri kwamba hatua ya kwanza katika kusuluhisha kiungulia ni kufuta kwenye meza na jiko lako vyakula vyote vinavyoongeza tatio kaka
  • Vyakula vilivyosindikwa na vyenye sukari kwa wingi+mafuta ya kupikia yalisosafishwa sana kiwandani
  • Pombe na vyakula vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa
  • Wanga kupita kiasi
  • Vinywaji vilivyoongezewa sukari kama soda na juisi za viwandani
  • Vyakula vulivyokaushwa kwa mafuta kama chips na viazi
  • Vyakula vyenye utindikali mwingi kama limau, nyanya, machungwa , tangawizi na kitungu maji. Badala yake hakikisha unakula
  • Vyakula vya mbogamboga kwa wigi hasa mboga za kijai, matangoo, kuku, nyama kutoka kwa mnyama laiyefugwa na kulishwa majani siyo nafaka, mafuta ya kupikia tumia mafuta ya nazi au mafuta ya mizeituni.
  • Tumia pia virutubisho kwa ajili ya kusaidia uchakataji wa chakula unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili kupata virutubisho.
  1. Weka ratiba ya kufanya mazoezi na kupunguza uzito na kitambi
    Maisha ya kizembe ya kutokushugulisha mwili ni chanzo cha uzito mkubwa na kitambi na magonjwa mengine lukuki ya lishe. Hakikisha unapata walau nusu saa kila siku kufanya mazoezi mepesi ili kuweka sawa uzito wako na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya lishe kama kisukari, kitambi, presha, upungufu wa nguvu za kiume, kuvurugika kwa homoni na mengine mengi.
  2. Epuka uvutaji wa sigara na kunywa pombe kupita kiasi
    uvutaji wa sigara na kunywa pombe unakuongeze hatari ya kupata kiungulia kutokana na kwamba vitu hivi vinaathiri misuli ya mfumo wa chakula na hivo kuongeza utolewaji wa tindikali.
  3. Kama tayari una shida ya kiungulia basi badili namna unavolala usiku
    Kama tulivoona kwenye somo letu hapo juu ni kwamba wagonjwa wa kiungulia hupata shida sana ya usingizi, jaribu zoezi hili. Kwenye kitanda chako upande unakoweka kichwa, chini ya godoro weka nguo ili kunyanyua kisi flani upande huo wa kichwa hii itakusaidia kupata nafuu. Jaribu pia kupata usingizi wa kutosha walau masaa 8 na kuendelea.

ANGALIZO WAKATI UNATIBU KIUNGULIA

Kama unagundua kwamba dalili za kiungulia zinajirudia kila mara japokuwa umefuata masharti haya yote ya lishe na mazoezi basi ni jambo jema kama ukimwona dactari akufanyie vipimo kujua pengine una tatizo kubwa la kiafya. Inawezekana kabisa tatizo la kiungulia kuwa kubwa pale unapokuwa kwenye matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi na baadhi ya vidonge vya kupunguza presha kwahiyo ni muhimu kupata ushauri wa dactari.

Dr Liwaya

Dar es salaam - Ilala boma

+255755162724 call/WhatsApp

+255717541527 call/WhatsApp

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.